Watu wote kanisani walipata nafasi ya kushiriki meza ya Bwana, na kabla hawajakula walipata nafasi ya kusema ni kitu gani wanataka Mungu awafanyie.
MAOMBEZI
Mara baada ya watu kula mkate (mwili wa Yesu ) na kunywa divai (Damu ya Yesu ) watu walianza kuanguka na kutapika na Mtumishi wa Mungu Nabii Frank alipita kwa kila mmoja kumuombea.
Sawa sawa na nguvu iliyowafungua watu siku ile jana nami natamka ukafunguliwe kutoka katika vifungo vya giza, laana , maagano , umaskini , kutokupata kazi , kushuka kila siku kiroho , kutokuendelea na masomo katika familia , kukosa kibali , biashara kutokuendelea na Mungu akakukumbuke wewe pamoja na familia yako tangu leo hata milele.
0 comments:
Post a Comment